HabariMastaaMengineyoSimulizi

Wachina Wagombea Kalio La Aunty Lulu! – Video

KATIKA hali ya kustajabisha, Wachina ambao hawakuweza kufahamika majina yao, wamenaswa wakipagawa na kugombea kumshika kalio, mtangazaji maarufu Bongo, Lulu Semagongo ‘Aunty Lulu’ nchini China.

Mrembo huyo amekwenda nchini humo hivi karibuni ambapo tukio hilo lilitokea alipohudhuria shoo ya mwanamuziki wa Tanzania anayeishi nchini humo aitwaye Zitha, iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Shenzhen.
Kwenye video ambayo Risasi Mchanganyiko liliipata, ilimuonesha Aunty Lulu akigombewa na Wachina hao huku wengine wakionekana kumrekodi video kupitia simu zao ambapo wengi walionekana kuvutiwa zaidi na kalio kubwa la Aunty Lulu.

Akiongea na Risasi Jumatano moja kwa moja akiwa nchini China, Aunty Lulu alisema alishangazwa na jinsi Wachina hao walivyomshobokea hadi akaogopa kwani kila mtu alikuwa akimvutia kwake.

“Unajua wameshangazwa na kalio langu huku wanawake wao hawana makalio hivi, niliona wanacheza nikainuka kucheza nao hilo lilikuwa ni kosa kwangu walipagawa ile mbaya,” alisema Aunty Lulu.

Aidha, Aunty Lulu alisema kuwa kilichomtisha ni jinsi Wachina hao walivyomgombea huku wengine wakiomba kupiga naye picha na wakati walipokuwa wakipiga naye picha, kila mmoja alikuwa akimgusa kalio.

“Nilikuwa nadhani naweza kujiachia kama kwetu Tanzania lakini kwa jinsi nilivyogombewa nitakuwa makini sana maana naogopa kubakwa,” alisema Aunty Lulu.

Akielezea safari yake ya China, Aunty Lulu alisema amekwenda nchini humo kibiashara ambapo amekwenda kwa ajili ya kuchukua vitu vya dukani.

Stori: Na Hamida Hassan, Risasi Mchanganyiko.

WACHINA WAGOMBEA KALIO LA AUNTY LULU! – VIDEO KATIKA hali ya kustajabisha, Wachina ambao hawakuweza kufahamika majina yao, wamenaswa wakipagawa na kugombea kumshika kalio, mtangazaji maarufu Bongo, Lulu Semagongo ‘Aunty Lulu’ nchini China. Mrembo huyo amekwenda nchini humo hivi karibuni ambapo tukio hilo lilitokea alipohudhuria shoo ya mwanamuziki wa Tanzania anayeishi nchini humo aitwaye Zitha, iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Shenzhen. Kwenye video ambayo Risasi Mchanganyiko liliipata, ilimuonesha Aunty Lulu akigombewa na Wachina hao huku wengine wakionekana kumrekodi video kupitia simu zao ambapo wengi walionekana kuvutiwa zaidi na kalio kubwa la Aunty Lulu. Akiongea na Risasi Jumatano moja kwa moja akiwa nchini China, Aunty Lulu alisema alishangazwa na jinsi Wachina hao walivyomshobokea hadi akaogopa kwani kila mtu alikuwa akimvutia kwake. “Unajua wameshangazwa na kalio langu huku wanawake wao hawana makalio hivi, niliona wanacheza nikainuka kucheza nao hilo lilikuwa ni kosa kwangu walipagawa ile mbaya,” alisema Aunty Lulu. Aidha, Aunty Lulu alisema kuwa kilichomtisha ni jinsi Wachina hao walivyomgombea huku wengine wakiomba kupiga naye picha na wakati walipokuwa wakipiga naye picha, kila mmoja alikuwa akimgusa kalio. “Nilikuwa nadhani naweza kujiachia kama kwetu Tanzania lakini kwa jinsi nilivyogombewa nitakuwa makini sana maana naogopa kubakwa,” alisema Aunty Lulu. Akielezea safari yake ya China, Aunty Lulu alisema amekwenda nchini humo kibiashara ambapo amekwenda kwa ajili ya kuchukua vitu vya dukani. Stori: Na Hamida Hassan, Risasi Mchanganyiko.

A post shared by Mapichapicha 2jiachie (@2jiachie) on

Facebook Comments

Tags
Show More

Related Articles

Close