MahusianoMastaaNews

Zari The Boss Lady: Natafuta Pesa, Sina Muda wa Kutafuta Mpenzi Mpya

SIKU chache baada ya mrembo Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ kutangaza kummwaga mpenzi wake, staa wa Bongo Fleva, Abdul Nasibu ‘Diamond Platnumz’, ameibuka na jipya tena huku safari hii akisisitiza kuwa wale wanaume wakware wote waliopanga foleni kusubiri penzi la Zari hawana nafasi kwani hana muda wa kuwa na mpenzi kwa sasa.

Zari alitangaza kumuacha mpenzi wake na Baba watoto wake staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz, mwezi uliopita lakini tangu hapo Kumekuwa na tetesi nyingi juu ya Zari kupata mwanaume mwingine wa kuchukua nafasi ya Diamond.

Kupitia kurasa yake ya SnapChat Zari ameweka wazi kuwa haitaji mpenzi kwa sasa baada ya marafiki zake kumtumia ujumbe uliosema;

“Kama mwanaume wako akienda kutafuta vimada wenye msambwanda mpya inabidi umkumbushe kuwa na wewe msambwanda wako mpya ni kwa ajili ya mwanaume mpya”.

Zari amedai kuwa marafiki zake wanamtumia meme hizo kama vijembe kwa EX wake lakini amejibu kuwa hataki mwanaume mpya kwa sasa:

“Marafiki zangu siwawezi hivi kwanini wamekazana kunionyesha hizi Mambo lakini hazinifai mimi….. Nahitaji kutafuta pesa mpya na sihitaji mwanaume kwa muda huu samahani!!!!”.

Facebook Comments

Tags
Show More

Related Articles

Close