Michezo

Simba Waendeleza Kichapo Dhidi Ya Prisons Bao 2-0

UMEMALIZIKA

DAKIKA 3 ZA NYONGEZA

Dk 90, Simba wanaonekana kugongeana taratibu kuonyesha wameridhika na bao hizo mbili

SUB Dk 88, Simba wanamtoa Okwi na nafasi yake inachukuliwa na Laudit Mavugo
Dk 85, Simba wanamtoa Zimbwe Jr na nafasi yake inachukuliwa na Nicholas Gyan
SUB Dk 83 Anatoka Chudu kwa upande wa Prisons anaingia John Sungura
GOOOOOOOOOOO Dk 80, Okwi anatumbia mpira wavuni na Kalambo anaanguka kulia, mpira unaingia kushoto
Dk 78 wachezaji Prisons kama vile hawafurahii, wanamzonga mwamuzi lakini anawaonya

SUB Dk 83 Anatoka Chudu kwa upande wa Prisons anaingia John Sungura
GOOOOOOOOOOO Dk 80, Okwi anatumbia mpira wavuni na Kalambo anaanguka kulia, mpira unaingia kushoto
Dk 78 wachezaji Prisons kama vile hawafurahii, wanamzonga mwamuzi lakini anawaonya

PENAAAAAAAATTT–KADI NYEKUNDU Dk 77, El Fadhil anamuangusha Bocco na mwamuzi anampa kadi ya pili ya njano na kuwa nyekundu
Dk 75 Kimenya anachonga kona nzuri, inapigwa vizuri…goal kick
Dk 74 Mlipili analazimika kulala na kuokoa na mpira unakuwa ni wa kurushwa, unarushwa na Kimenya na kuwa kona
SUB Dk 72 Kotei anaingia kuchukua nafasi ya Kwasi ambaye ameumia na kutolewa na machela na kupelekwa vyumbani
Dk 70, Simba wanagongeana vizuri, Kapombe anampa Okwi, naye anamuachia Kichuya anaachia shuti ndizi linagonga mwamba na kurudi uwanjani


Dk 62, Kalambo wa Prisons anafanya kazi ya ziada kuokoa shuti kali na kuwa kona, inapigwa inaokolewa
Dk 59, Prisons wameamka usingizini, wanaonekana kushambulia mfululizo katika lango la Simba
KADI Dk 57 Mkude analambwa kadi ya njano kwa mchezo wa kibabe
Dk 56 mpira wa adhabu wa Okwi unapita juu kidogo ya lango la Prisons, goal kick

Dk 55, Bocco anaanguka nje kidogo ya eneo la 18 na unawekwa mpira wa faulo
Dk 53 Eliuta Mpepo anachambua na kuachia mkwaju lakini unakuwa nyanya katika mikono ya Manula

Dk 50 Kichuya anamhadaa vizuri beki Prisons, anaachia mkwaju wa kimo cha nyoka, goal kick
Dk 49, Prisons wanaonekana wamefunguliwa kucheza undava, Bocco anaonekana kuchukizwa na hiyo hali
Dk 48 inachongwa tena, kipa anaokoa, Nyoni anamtengea Mkude, anapiga shuti kuuuubwaaaa
Dk 48 Kona ya Kapombe, kipa anaokoa na El Fadhil na kuwa kona nyingine

Dk 47 Kapombe anaingiza krosi matata, Mwasote anawahi mbele ya Bocco, anautoa na kuwa kona ya kwanza kipindi cha pili
Dk 46 Prisons wanakuwa wa kwanza kufika katika lango la Simba lakini Manula yuko makini
Dk 45 Mpira umeanza na Simba wameanza kwa kushambulia, Prisons wako makini

MAPUMZIKO

-KADI Kadi ya njano kwa Jumanne El Fadhil kwa kumrukia MKude
DAKIKA 2 ZA NYONGEZA
Dk 44, mpira wa adhabu wa Kichuya, Okwi anapiga kichwa lakini Kalambo anapangua na Mwasote anaosha
SUB Dk 43 Prisons wanamtoa Mkandala nafasi yake inachukuliwa na Ibata

Dk 42, Simba wanaingia tena eneo la hatari la Prisons, Bocco anaachia shuti, Kalambo anadaka
Dk 40 kuna mchezaji wa Prisons anatolewa nje, hii ni mara ya pili, inaonekana hayuko vizuri au aliumia pale baada ya kugongwa na Juuko Murshid
Dk 39 Okwi katika sehemu nzuri, anaachia shuti lakini kuuuubwaaa
Dk 37, Simba wanaingia tena, hatariiiii ni Okwi lakini kipa anadaka vizuri mpira wake wa krosi
GOOOOOOOOOOOOOO Dk 35, Bocco anapiga kichwa na kuujaza wavuni mpira uliogonga mwamba na kurudi baada ya krosi safi ya Nyoni aliyempindua beki Prisons

Dk 34, Kapombe naingia, kona nyingine inachongwa na kuokolewa, inachongwa na Kichuya kona tena. Inachongwa inaokolewa tena lakini bado
Dk 32, krosi nyingi safi ya Kapombe, Mwasote anaokoa na kuwa kona. Kona ya sita inachongwa hapa, goal kick
DK 29, Okwi anapokea pasi nzuri ya Bocco, anapiga inazuiliwa, anampa Kichuya anapiga Kalambo anadaka vizuri kabisa
Dk 27, Bado mpira hauvutii sana na hakuna mashambulizi makali zaidi ya pasi nyingi katikati ya uwanja
Dk 23 Eliuta Mpepo anajaribu shuti katika lango la Prisons lakini hakulenga

Dk 23,kona safi inachongwa hapa, Bocco anapiga, Prisons anaokoa inakuwa kona ya tano, inachongwa na Kwasi na Kalambo anadaka kwa ulaini kabisa
Dk 22, Pasi nzuri ya Kichuya, Bocco anawahi na kuchonga krosi, Chona anaokoa na kuwa kona
Dk 20, Jonas Mkude anatolewa nje baada ya kugongwa na beki wa Prisons wakiwania mpira
Dk 19 mpira si ule wenye kasi sana na inaonekana wachezaji wanacheza kwa tahadhari kubwa na hii inaondoa ule mvuto wa uchezaji

Dk 18, mpira wa kona ya chini ya Simba unaokolewa na Chona
Dk 17, Simba wanapata kona baada ya shambulizi na inachongwa na Kapombe
Dk 14 sasa, bado hakuna timu yenye mipango madhubuti inayoonyesha kuna dalili nzuri za kupata bao
Dk 11, kona inachongwa na Kapombe lakini Kalambo anaruka na kudaka vizuri kabisa
Dk 10, Okwi anaingia vizuri kabisa hapa lakini Prisons wanaokoa na kuwa kona

Dk 7 Mohammed Rashid anamuacha vizuri Kapombe lakini Juuko anamtuliza kwa kumlaza chini
Dk 5, pasi nyingi wanapiga Simba na Prisons wanaonekana wamerudi kuhakikisha hawaruhusu mipira kupita
Dk 3 Kichuya nje ya 18 anajaribu tena lakini Prisons wako makini
Dk 2 Kapombe anaingiza kona ile, Asukile anaokoa lakini Kalambo anatokea na kudaka vizuri kabisa
Dk 1, Simba wanajibu shambilizi, krosi ya Kichuya hatarii, Kalambo anaokoa na kuwa kona
Dk 1, mechi inaanza na Prisons wanaanza kwa kasi wakicheza kwa kujiamini tartiiibu

Facebook Comments

Tags
Show More

Related Articles

Close