MahusianoMastaaMASTAA WA BONGO

Diamond Platnumz na Irene Waonekana Pamoja Zanzibar (+picha)

Staa wa muziki wa Bongo fleva na CEO wa WCB, Diamond Platnumz amedaiwa kuonekana kwenye visiwa vya Zanzibar akiwa na video queen Irene Hillary.

Diamond ambaye alitangaza kuwa yupo Single wiki iliyopita baada ya kuachana na mpenzi wake wa siku nyingi na mama watoto wake Hamisa Mobetto, ameonekana kupata mpenzi mwingine.

Kwa muda mrefu kumekuwa na tetesi kuwa Diamond ana Mahusiano ya Kimapenzi na Irene mpaka kuna muda ilisemekana kuwa aliwahi kubeba ujauzito wake.

Diamond ambaye kwa sasa yupo visiwani Zanzibar kwa ajili ya kazi zake za sanaa anadaiwa kuonekana na Mrembo Irene wakiwa bega kwa bega kuonyesha kuwa wako pamoja.

Picha ambayo inasambaa Kwenye mitandao ya kijamii inawaonyesha wawili hao wakiwa pamoja na crew nzima ya WCB:

Facebook Comments

Tags
Show More

Related Articles

Close