BurudaniMahusianoMastaa

Madee: Dogo Janja na Irene Uwoya Hawajaachana

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Madee Ali amefungukia Mahusiano ya Msanii mwenzake Dogo Janja na Mke wake staa wa Bongo movie Irene Uwoya.

Madee ambaye ni Baba Mlezi wa Dogo Janja ameibuka na kupiga chini tetesi hizo ambazo zimekua zikipamba moto Kwenye mitandao ya kijamii.

 

Madee amedai na yeye mwenyewe anachangazwa na taarifa hizo kuzagaa mitandaoni, kwa watu kuongea masuala mengi juu ya ndoa hiyo bila ya kuwa na uhakika wa jambo husika.

Dogo Janja na Irene Uwoya hawajaachana nani amesema wameachana?, sidhani kama kuna kitu chochote kimewakuta ila ninachojua mimi wapo sawa, hadi dakika hii tunayozungumza na wapo pamoja kabisa”.

Siku za hivi karibuni kumekuwa na tetesi kuwa wanandoa Irene na Dogo Janja wanaelekea kupeana talaka baada ya kusemekana Uwoya kupata danga lenye pesa ndefu.

Facebook Comments

Show More

Related Articles

Close